Jumatatu 7 Septemba 2026 - 12:16
Kusini Mwa Lebanon ni Nguzo Muhimu Zaidi ya Muundo wa Mfumo wa Utawala;Serikali Isiyoilinda Imeiuza Nchi

Hawza/ Sheikh Ahmad Qabalan, Mufti Mashuhuri wa Jaafari, akimuelekea Rais wa Lebanon amesema: “Uwezekano wa mgawanyiko wa ndani umefikia kiwango cha juu kabisa, na wewe una wajibu wa kuzuia kusambaratika taifa, si kuongeza zaidi mgawanyiko huo.”

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ahmad Qabalan, mwanazuoni wa Kishia na Mufti Mashuhuri wa Jaafaria, ametoa ujumbe katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka mitano tangu kufariki dunia Ayatullah Sheikh Abdul-Amir Qabalan, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon.

Sheikh Ahmad Qabalan kumuelekea Rais wa Lebanon: Hatari ya Mgawanyiko wa Ndani Imefikia Kiwango cha Juu, Na Una Wajibu wa Kuzuia Kusambaratika kwa Taifa

Sheikh Ahmad Qabalan, akimuelekea Rais wa Lebanon, Jenerali Joseph Aoun, amesema: “Uwezekano wa mgawanyiko wa ndani umefikia kiwango cha juu kabisa, na wewe una wajibu wa kuzuia kusambaratika kwa taifa, si kuongeza zaidi mgawanyiko huo. Jambo hili linahitaji ushirikiano na mshikamano wa mamlaka za dola, uadilifu, kuaminiana kitaifa na uwepo madhubuti wa taasisi zote za serikali ndani ya moyo wa Kusini, hususan katika eneo linalokaliwa kwa mabavu.” Amesema kwamba jukumu la mamlaka ya dola katika eneo hilo linapitia kwenye kuulinda muundo wa kitaifa na uwepo wa Lebanon, kutoka ndani na nje.

Akirejelea msimamo wa Sheikh Abdul-Amir kuhusu dhana ya msingi ya taifa, alisema kwamba, Sheikh huyo aliifupisha kwa kauli yake kwa kusema: “Hakuna madhehebu wala ahadi yoyote ya nje inayoweza kuwa juu ya ahadi za makubaliano ya kitaifa na mikataba yake ya kimsingi, na hakuna jambo muhimu zaidi kuliko kuaminiana kitaifa.”

Akaongeza kwamba; kuaminiana kitaifa kunamaanisha kukataa kuwaondoa wengine katika mfumo wa taifa. Hata hivyo, wapo wanaotaka kutuondoa, na sisi tutajilinda kwa nguvu kubwa zaidi ya kitaifa.

Kusini mwa Lebanon ni Nguzo Muhimu Zaidi ya Muundo wa Mfumo wa Utawala; Kuilinda Kusini Kunahitaji Serikali Imara Ndani ya Kusini

Aliendelea kusema: “Ninalisema hili kwa ajili ya historia: Kusini ni nguzo muhimu zaidi ya kimsingi katika muundo wa mfumo wa utawala, na kuilinda Kusini mwa Lebanon kunahitaji uwepo kwa serikali yenye nguvu ndani ya moyo wa Kusini.”

Alisema kuwa, hatari ipo katika mamlaka ambayo imeacha kutekeleza jukumu lake la kitaifa, na kwamba thamani ya Muqawama inaonekana wazi katika eneo hili; Muqawama ambao unalilinda utaifa na serikali, wakati serikali yenyewe haitaki kuunga mkono Muqawama huo na inatekeleza mfumo wa pande tatu kwa lengo la kuondokana na nguvu kubwa zaidi ya kitaifa ya mamlaka iliyokuwepo katika kipindi cha miongo kadhaa iliyopita.

Ni katika mazingira hayo, alisema, ambapo Sheikh Abdul-Amir alikuwa akisema: “Israel ni utawala wa kigaidi, na hatari yake haipo tu katika mipaka, bali pia kwa yule anayefanya uwekezaji ndani ya Lebanon kwa ajili yake.”

Kwa maana hiyo hiyo, alisema: “Kuilinda Lebanon ni wajibu muhimu zaidi wa kitaifa, na Muqawama unafanya kazi ambayo serikali haiifanyi.”

Kwa mtazamo huo, Muqawama unalinda mamlaka ya kitaifa na si mbadala wa serikali. Isipokuwa kwamba hakuna serikali yenye mamlaka kamili ya kitaifa, na hivyo nguvu zote za kitaifa zinapaswa kujenga mamlaka yenye uwezo wa kulinda taifa ambalo halitakubali kuwa tegemezi kwa mtu yeyote.

Amesema kuwa leo Muqawama unailinda nchi, serikali na taasisi zake, na unafanya juhudi za muda mrefu zinazotokana na kujitolea na kujitoa mhanga kwa ajili ya mamlaka ya kitaifa.

Akaongeza kuwa; kinachotakiwa ni kuikomboa Lebanon kutoka katika mipango ya kuiuza na kuhalalisha hati na nyaraka za uuzaji huo, na kupitisha sera itakayozuia kusambaratika kwa nchi kutokea ndani.

Alisisitiza kwa kusema: “Hatutanyamaza mbele ya sera inayogeuza hofu kuwa mipango, inayolinyamazisha na kulikandamiza kundi zima la kimadhehebu, na kutumia tena mamlaka kama chombo cha kuhudumia mradi wa Marekani kwa kutumia fursa nchini.”

Kwa mujibu wa mantiki ya Sheikh Abdul-Amir, alisema, bila kuwepo mamlaka yenye msingi wa makubaliano na umoja wa ndani, nchi itasambaratika, na mamlaka inayopoteza msingi wake wa makubaliano ya kitaifa hupoteza jukumu lake la kitaifa.

Akaendelea kusema: “Kinachotakiwa ni kurejesha maslahi ya kitaifa, na mamlaka ya Kusini ndiyo mtihsni muhimu zaidi wa kuipima serikali. Kinachotakiwa ni kurejeshwa eneo linalokaliwa kwa mabavu ndani ya Kusini mwa Lebanon kwa Lebanon, si kwa Wazayuni na mradi wao wa kiusalama.”

Sheikh Ahmad Qabalan: Lebanon ni Moja, Hakuna Lebanon Mbili

Sheikh Ahmad Qabalan, akimuelekea Rais Aoun, amesema: “Upande mwingine wa Lebanon ni mshirika wako mwanzilishi katika nchi hii. Lebanon ni moja, na hakuna Lebanon mbili. Kumlinda mwingine ni sehemu ya kujilinda mwenyewe, na kuilinda Kusini ni sehemu ya kuilinda Beirut na Baabda.” Amesema kwamba, serikali haiko nje ya dhana ya msingi ya kitaifa, na kwamba mamlaka yoyote inayopinga ukweli huu inafanya “mauaji ya kitaifa ya kujidhuru.”

Aliongeza kusema: “Wakati mamlaka ya Lebanon inapoihitajia Washington ili ilindwe, itakuwa imepoteza jukumu lake.” Aidha, alisema: “Hakuna jambo lililo hatari zaidi kwa Lebanon kuliko ‘kuuawa kwa uraia wa kisiasa’, na wapo wanaoufanya uraia huo kuuawa.”

Kwa mujibu wa Sheikh Qabalan, makubaliano ya mfumo wa pande tatu hayakuiba tu usalama kutoka katika eneo linalokaliwa kwa mabavu, bali yaliipora Lebanon nzima, na kuinyang’anya serikali iliyojisalimisha sifa yake ya kuwa serikali ya kitaifa.

Akasema: “Hakuna usaliti mkubwa zaidi kwa nchi hii kuliko kusaliti dhana ya taifa, mwananchi na mamlaka ya Kusini.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha